KWA HILI YANGA WAPASWA KUIGA KWA SIMBA

Kilichofanywa na Simba SC ni kitu kikubwa sana katika mpira wetu Tanzania na ni jambo la kupongezwa na kuigwa.
Ulimwengu wa soka hivi sasa unasimama katika misuli bora ya kiuchumi. Watu wenye nguvu za kiuchumi na weledi sahihi wa kuuendesha mpira kibiashara ndio watu sahihi kulishika soka letu. Kikubwa Simba ya Mohamedi Dewji ni kusimama vyema kama kielelezo cha soka la kisasa nchini ili vilabu vingine viige na hatamu bora kisoka tuikamate nchini.
Big up Simba SC ! leo mmedhihirisha nini maana ya kauli mbiu yenu NGUVU MOJA . Ni nguvu ambayo imelenga katika umoja, ushirikiano, weledi na matamanio chanya kuleta mapinduzi sahihi ya soka nchini.
Maamuzi mliyofikia leo endapo LENGO litatimia basi kumbukumbu yenu itajichora kwa wino wa chuma kusomwa na vizazi vingi vijavyo si kwa Simba tu bali kwa watanzania wote katika tasnia ya soka nchini.
Neno langu kwenu;
samuel samuel

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF