MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF

Mbeya city wakata rufaa bodi ya ligi maamuzi ya mechi yao na Simba SC jumapili ya tarehe 5 November 2017. Rufaa hiyo inaelezea kutoridhishwa na goli walilofungwa dakika ya 7 na Shiza Kichuya. Wanalilalamikia kwamba ni goli la kuotea !
Note
Uongozi wa timu ya Mbeya City umeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulalamikika kutotendewa haki katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.
Mbeya City ilichapwa 1-0 Jumapili na Simba, bao pekee la Shiza Ramadhani Kichuya katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema kwamba uchezeshaji wa refa Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Omar Juma wote wa Dodoma na Michael Mkongwa kutoka Njombe haukuwa wa haki kwa mujibu wa sheria 17 za soka.
Bin Zubery

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965