UKIMYA MBINU MPYA SIMBA NA YANGA?
UKIMYA MBINU MPYA SIMBA NA YANGA?!.... Ni nadra sana kuelekea mpambano wa watani wa jadi kukosa shamra shamra , tambo , mbwembwe na kila aina ya vituko ili mradi kila mmoja kujinasibu ni bingwa kuliko mwenzake. Majigambo kwa viongozi hususani wasemaji wa timu pia mashabiki yamepungua sana na ukimya umetawala kwa kambi zote . Kilichobaki ni kalamu za waandishi na sauti za watangazaji kujaribu kuinadi derby hiyo. Mara nyingi ratiba ya ligi inapotoka wengi huvutiwa zaidi kutazama tarehe ya watani wa jadi kukutana na kuanza kutambiana. Tambo ambazo huanzia kwenye kipindi cha usajili na mechi za awali. Lakini msimu huu joto la watani wa jadi kwa majigambo na mbwembwe za kila aina zimepotea. Msimu uliopita wa 2015-16 kidogo tambo zilikuwa kali lakini zikizaa tawi jipya la watani hao wa jadi nje ya timu hizo kongwe zaidi nchini . Wasemaji wa vilabu hivyo yaani Jerry Muro kwa Yanga SC na Haji Manara kwa Simba SC waliibuka videdea kwa kusuguana zaidi kwa tambo za utani wa jadi kuliko t...