Posts

KWA HILI YANGA WAPASWA KUIGA KWA SIMBA

Image
Kilichofanywa na Simba SC ni kitu kikubwa sana katika mpira wetu Tanzania na ni jambo la kupongezwa na kuigwa. Ulimwengu wa soka hivi sasa unasimama katika misuli bora ya kiuchumi. Watu wenye nguvu za kiuchumi na weledi sahihi wa kuuendesha mpira kibiashara ndio watu sahihi kulishika soka letu. Kikubwa Simba ya Mohamedi Dewji ni kusimama vyema kama kielelezo cha soka la kisasa nchini ili vilabu vingine viige na hatamu bora kisoka tuikamate nchini. Big up Simba SC ! leo mmed hihirisha nini maana ya kauli mbiu yenu NGUVU MOJA . Ni nguvu ambayo imelenga katika umoja, ushirikiano, weledi na matamanio chanya kuleta mapinduzi sahihi ya soka nchini. Maamuzi mliyofikia leo endapo LENGO litatimia basi kumbukumbu yenu itajichora kwa wino wa chuma kusomwa na vizazi vingi vijavyo si kwa Simba tu bali kwa watanzania wote katika tasnia ya soka nchini. Neno langu kwenu; samuel samuel

SIMBA KUIBANIA SINGIDA UNITED KWA LUZIO?

Image
HARAKATI za klabu ya Singida United ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi hawataki kumuachia. Singida inamuhitaji Liuzio kwa ajili ya kuongezea nguvu kikosi chake kwenye mzunguko wa pili baada ya kurizishwa na kiwango chake. Rafiki wa karibu wa Liuzio aliiyambia Mkalimangi blog, ni kweli Singida wanamuhitaji mchezaji huyo lakini Simba imeonyesha dalili zote kuwa haitaki kumuachia. "Kweli Singida inamtaka, Liuzio lakini Simba wamegoma, hawataki kumtoa sasa sijui kwa nini wakati wenyewe hawampi nafasi kubwa ya kucheza. Bora wangemtoa akajaribu maisha mengine huko,"alisema. Liuzio mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, klabu iliyomlea na kumuuza Zesco ya Zambia, alirudi nchini mwaka jana akasajiliwa kwa mkopo na Simba anayoichezea mpaka sasa

MTAZAMO WA MDAU KUHUSU NGOMA DONALD

Image
Huu ulikuwa usajili makini msimu wa 2015-16 lakini haukuwa usajili sahihi kwa msimu huu. Commitment ni kitu cha msingi sana kazi huonesha heshima na uwajibikaji. Kuna wakati wafanyakazi hutakiwa kulinda ajira zao na masilahi mapana ya taasisi wanayoitumikia. Fedha iliyotumika katika usajili ilipaswa kutafuta wachezaji wenye nidhamu, kujituma , wavumilivu na wenye kuheshimu masilahi ya timu. Ni ukweli usiopingika Ngoma ni mmoja kati ya wachezaji wenye kipaji kikubwa kumvutia  mwalimu yoyote yule lakini anakosa kitu cha msingi sana kulinda kipaji chake ; nidhamu. Huwezi kuondoka eneo la kazi bila kibali sahihi cha kiongozi wako lakini pia kuitikia wito nakuonesha kujali ni jambo lingine ambalo linachangia katika uwajibikaji. Yawezekana kabisa klabu ikawa haijamtendea haki katika matibabu yake kulingana na uhitaji sahihi wa matibabu ya jeraha husika lakini kuonesha nidhamu na kujali kile kidogo ambacho klabu inajituma katika ukata mgumu kama huu ni jambo la kushuku...

HUYU NDO PATO NGONYANI ALEWATOA MCC KIJASHO

Image
PATO NGONYANI AIPA YANGA GOLI 9! Moja ya nafasi ngumu katika soka ni kiungo cha chini. Hii ndio nafasi ambayo inaleta uwiano wa timu katika kujilinda na kushambulia. Roy Keane moja ya viungo bora kuwahi kutokea duniani akitamba sana na kikosi cha Manchester United eneo la kiungo cha chini aliwahi kusema ; " kiungo mkabaji ndio moyo wa timu. Ubora wake uwanjani unawafanya wenzake kutimiza vyema majukumu yao uwanjani " Kwa mtazamo huo, Pato Ngonyani amekuwa na mchezo mzuri kila anapopata nafasi ya kucheza na kutimiza majukumu yake kama ' moyo wa timu'. Pato Ngonyani huu ni moja ya viungo wa Yanga ambaye hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza . Ana wastani wa kucheza mechi kati ya 3 mpaka 7 katika mzunguko wa mechi 30 katika ligi kuu. Licha ya uchache huo ameendelea kuaminika katika kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini kutokana na uwezo wake uwanjani anapopata nafasi. Yanga SC msimu huu wamekuwa na tatizo kubwa la majeruhi na wachezaji ...

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

Image
MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965 Young Africans SC mara 27 Simba SC mara 18 Mtibwa Sugar mara 2 Mseto mara 1 Cosmopolitan mara 1 Coastal Union 1 Tukuyu 1 Pan Africans mara 1 Azam mara 1 Kuanzia mwaka 1965 mpaka 1982 ligi hii ilikuwa ikijumuisha timu za Tanzania bara na visiwani baada ya hapo kila shirikisho kuendelea na ligi yake, FAT ( sasa TFF ) kwa upande wa Tanzania bara na ZFA kwa upande wa Zanzibar. Kwa mtazamo huo Young Africans wanabaki mabingwa wa kihistoria nchini. Ligi hii mwanzoni ilijulikana kama ligi daraja la kwanza ( sasa ligi kuu ) Na samuel samuel

USAJIRI YANGA KATIKA DIRISHA DOGO UZINGATIE HAYA

Image
MTAZAMO WA DIRISHA DOGO LA USAJILI NA TIMU 16 ZA LIGI KUU ....inaendelea MTAZAMO WA Mwanasoka SAMUEL SAMUEL 2. Yanga SC Hawa ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara tatu mfululizo wakifanya hivyo 2014-15, 2015-16 na 2016-17 lakini pia wakisimama kama mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo kwa mara 27 toka kuanzishwa kwake mwaka 1965 . Kwa misimu kadhaa Yanga SC wamekuwa vyema katika usajili kwa maana ya kuandaa timu nzuri katika mapambano ya ligi hii ndio maana kwa sehemu kubwa wameweza kuitawala ligi kwa muda mrefu ingawa changamoto kubwa ni michuano ya kimataifa . Msimu huu wa 2017-18 ni moja ya msimu ambao mabingwa hawa hawakufanya usajili wa kutisha kama ilivyo ada zaidi ya kurekebisha mikataba ya wachezaji waliopo , kuziba mapengo muhimu yenye ulazima mkubwa mfano eneo la kiungo walipowanasa Pappy Tshishimbi toka Congo, Rafael Daudi wa Mbeya City, Piusi Buswita wa Mbao FC na kiungo huru Buruan Yahya . Sambamba na hilo ni kuimarisha safu ya ulinzi kwa kums...

TIMU ZIFANYE HAYA KATIKA DIRISHA DOGO LA USAJIRI ILI KUJIWEKA SAWA

Image
SAMUEL SAMUEL  MTAZAMO WA TIMU 16 ZA LIGI KUU KATIKA DIRISHA DOGO LA USAJILI Naanza na Simba SC Eneo la ulinzi Dirisha dogo la usajili hawana kazi kubwa sana katika eneo hili ni kiasi cha kutathimini majeruhi ya Shomari Kapombe na mustakabali wao kama timu hususani kwenye mechi za kimataifa kombe la Shirikisho. Ubora wa Erasto kulia sambamba na Ally Shomari bado wanaweza kuliziba vyema pengo lake . Erasto ni moja ya usajili makini ambao Simba walifanya; kimbinu ni mchezaji kiraka kutawala eneo lote la nyuma pia kiungo cha chini. Eneo la kiungo Ni eneo ambalo wapo vyema sana kuliko eneo lolote lakini kuna mabadiliko yanatakiwa kufanyika . Siioni nafasi ya Jamali Mnyate ndani ya klabu hiyo. Huyu wamtoe kwa mkopo kufungua nafasi ya wengine au kubaki na wachezaji wachache ambao kocha anaweza kuwatumia vyema . Ndemla kama atafanikiwa Sweden ni jambo la kheri ili kijana Mohamedi Ibrahim apate nafasi ya kucheza . Muunganiko wa Mkude, Kotei , Muzamiru , Ibrahim, Kichuya na Har...