HUYU NDO PATO NGONYANI ALEWATOA MCC KIJASHO
PATO NGONYANI AIPA YANGA GOLI 9!
Moja ya nafasi ngumu katika soka ni kiungo cha chini. Hii ndio nafasi ambayo inaleta uwiano wa timu katika kujilinda na kushambulia.
Roy Keane moja ya viungo bora kuwahi kutokea duniani akitamba sana na kikosi cha Manchester United eneo la kiungo cha chini aliwahi kusema ; " kiungo mkabaji ndio moyo wa timu. Ubora wake uwanjani unawafanya wenzake kutimiza vyema majukumu yao uwanjani "
Kwa mtazamo huo, Pato Ngonyani amekuwa na mchezo mzuri kila anapopata nafasi ya kucheza na kutimiza majukumu yake kama ' moyo wa timu'.
Pato Ngonyani huu ni moja ya viungo wa Yanga ambaye hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza . Ana wastani wa kucheza mechi kati ya 3 mpaka 7 katika mzunguko wa mechi 30 katika ligi kuu. Licha ya uchache huo ameendelea kuaminika katika kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini kutokana na uwezo wake uwanjani anapopata nafasi.
Yanga SC msimu huu wamekuwa na tatizo kubwa la majeruhi na wachezaji ambao wamekuwa wakisimamishwa kutokana nakuwa na kadi tatu za njano. Mchezo wa Yanga na Stand United mjini Shinyanga Pato alipata nafasi ya kucheza mchezo huo baada ya kiungo Thabani Kamusoko kuumia akisimama vyema na Pappy Tshishimbi aliyecheza juu kama namba nane.Pato aliweza kusimama imara eneo la kiungo na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa goli nne (4) akisaidiana na viungo wenzake.
Uwezo wa kumiliki mpira, kusambaza mpira kwa wakati , kukaba na kuhakikisha hatengenezi nafasi tupu juu yake , ndivyo vinamfanya kiungo huyu mkabaji mzawa kuna na uwezo mzuri kutunza muhimili wa timu kuanzi eneo la kati.
Mchezo wa jana ( jumapili ) dhidi ya Mbeya City , Pato akitengeneza muhimili mzuri eneo la kati sambamba na viungo wenzake waliweza kuipatia Yanga goli tano (5) dhidi ya timu hiyo toka nyanda za juu kusini.
Zaidi ya magoli mawili yalianzia kwake kwa maana ya uwezo wake kutengeneza daraja zuri kiufundi na Rafael Daudi aliyekuwa anasambaza mipira juu.
Mara nyingi viungo wa chini wakicheza hovyo hurusu timu pinzani kuwashambulia kupitia njia ya kati ( pressing ) lakini uimara wa defensive midfielder, kiungo mchezeshaji na playmaker wa juu huhifanya timu kuwa tactically balanced.
Bado ana mapungufu ambayo yanamfanya kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza lakini ni moja ya viungo wazawa wenye kipaji halisi eneo hilo la kati. Anahitajika kuongeza kasi kwenye ' give and go passes ' ( holding ) , kukabia juu kwa maana ya kukataa kusukumwa nyuma hali inayowafanya walinzi wa kati kukosa anticipation nzuri ya kukaka .
Kucheza mara kwa mara kutazidi kuimarisha kipaji chake !.
Samuel Samuel

Comments
Post a Comment