TIMU ZIFANYE HAYA KATIKA DIRISHA DOGO LA USAJIRI ILI KUJIWEKA SAWA

SAMUEL SAMUEL 
MTAZAMO WA TIMU 16 ZA LIGI KUU KATIKA DIRISHA DOGO LA USAJILI
Naanza na Simba SC
Eneo la ulinzi
Dirisha dogo la usajili hawana kazi kubwa sana katika eneo hili ni kiasi cha kutathimini majeruhi ya Shomari Kapombe na mustakabali wao kama timu hususani kwenye mechi za kimataifa kombe la Shirikisho. Ubora wa Erasto kulia sambamba na Ally Shomari bado wanaweza kuliziba vyema pengo lake . Erasto ni moja ya usajili makini ambao Simba walifanya; kimbinu ni mchezaji kiraka kutawala eneo lote la nyuma pia kiungo cha chini.
Eneo la kiungo
Ni eneo ambalo wapo vyema sana kuliko eneo lolote lakini kuna mabadiliko yanatakiwa kufanyika . Siioni nafasi ya Jamali Mnyate ndani ya klabu hiyo. Huyu wamtoe kwa mkopo kufungua nafasi ya wengine au kubaki na wachezaji wachache ambao kocha anaweza kuwatumia vyema . Ndemla kama atafanikiwa Sweden ni jambo la kheri ili kijana Mohamedi Ibrahim apate nafasi ya kucheza . Muunganiko wa Mkude, Kotei , Muzamiru , Ibrahim, Kichuya na Haruna ndio ' pride ' ya Simba . Lakini ni wakati wa kuwaongeza mikataba Muzamiru na Kichuya kama bado hawajafanya hivyo maana inakwenda ukingoni.
Ushambuliaji
Hili ndio eneo ambalo kamati ya usajili na kocha mkuu wa Simba wanatakiwa kuwa makini sana kipindi hiki cha usajili. Yafanyike maamuzi magumu juu ya Laudit Mavugo ; avunjiwe mkataba kama walivyofanya Azam FC kwa Yahya na kutafuta mchezaji wa kigeni mwenye ubora mzuri kama mshambuliaji kiongozi. Boko ni mzuri kwa pacha yake na Okwi lakini majeruhi na soka lake kuelekea ukingoni anakosa consistency nzuri ya kupambania timu kila mechi . Simba wakitulia na kupata mpachika mabao mwenye wastani wa 1:1 asie na aibu na goli watafika mbali na wanaweza kubeba kombe la ligi kuu msimu huu pia kufika mbali michuano ya Shirikisho .
Wajitafakari pia kwa Nicolas Gyan; huyu mshambuliaji toka Ghana sijaona mchango wake chanya Simba SC toka atue nchini kama ilivyo kwa Emanuel Okwi . Kama terms za mkataba zina kipengele cha ' ufanisi ' ni wazi Simba wamfungulie mlango wa kutokea . Wapo wazawa bora zaidi yake lakini si Luizio huyu nae hatoshi kuwepo Msimbazi .
Kama Gyan na Mavugo wataondoka na kamati ya usajili ikapata wachezaji wazuri wakigeni ( matured ) basi timu inaweza kuwa bora eneo hilo.
Kikubwa Simba wanahitajika kusimama imara kwenye kauli mbiu yao NGUVU MOJA ili kuijenga timu yenye ushindani mkubwa katika michuano iliyo mbele yao hususani kombe la Shirikisho. Kama klabu kipindi hiki cha usajili waitathimini timu kwa viwango vya vilabu watakavyokutana navyo katika michuano ya kombe la Shirikisho ili wajue ubora wao na mapungufu yao.
@Samuel Samuel

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF