MTAZAMO WA MDAU KUHUSU NGOMA DONALD
Huu ulikuwa usajili makini msimu wa 2015-16 lakini haukuwa usajili sahihi kwa msimu huu. Commitment ni kitu cha msingi sana kazi huonesha heshima na uwajibikaji. Kuna wakati wafanyakazi hutakiwa kulinda ajira zao na masilahi mapana ya taasisi wanayoitumikia. Fedha iliyotumika katika usajili ilipaswa kutafuta wachezaji wenye nidhamu, kujituma , wavumilivu na wenye kuheshimu masilahi ya timu.
Ni ukweli usiopingika Ngoma ni mmoja kati ya wachezaji wenye kipaji kikubwa kumvutia mwalimu yoyote yule lakini anakosa kitu cha msingi sana kulinda kipaji chake ; nidhamu.
Huwezi kuondoka eneo la kazi bila kibali sahihi cha kiongozi wako lakini pia kuitikia wito nakuonesha kujali ni jambo lingine ambalo linachangia katika uwajibikaji.
Yawezekana kabisa klabu ikawa haijamtendea haki katika matibabu yake kulingana na uhitaji sahihi wa matibabu ya jeraha husika lakini kuonesha nidhamu na kujali kile kidogo ambacho klabu inajituma katika ukata mgumu kama huu ni jambo la kushukuru sana.
Yanga imeingia mkataba wa mwaka na Amisi Tambwe ambaye hajacheza hata mechi moja lakini amekuwa akipata stahiki zake hata kama kwa kuchelewa mbona, hii yote inaonesha uvumilivu wa klabu hiyo kwa watumishi wake.
Yanga inahitajika kutazama thamani ya klabu yao na utumishi wa wachezaji wake . Huwezi kuingia signing fee ya almost 40,000 USD bado ukashindwa kuthamini masilahi ya timu.
Replacement is needed
SAMUEL SAMUEL
Comments
Post a Comment