Posts

MACHUNGU YA WANASIMBA TETESI ZA MO KWENDA YANGA

Image
kumbukwe kwa sasa Mohamed Ibrahim almaharufu kama "MO" wanavyopenda kumuita Wanamsimbazi hao amekuwa guzo kubwa mitandaoni na hata kwenye vyombo mbalimbali vya habari akihusishwa kutimkia Yanga Sc ambao wanahitaji huduma ya mchezaji huyo tokea akiwa Mtibwa Sugar ya pale Morogoro inayocheza ligi kuu. Kutokana na Sintofahamu inayoendelea ndani ya Simba na hata kwa mchezji mwenyewe inaonyesha MO akiwa na furaha japo kuna picha mbalimbali zikimuonyesha kama MO amekuwa hana furaha ndani ya Wekundu wa Msimbaza. Kutokana na hali hiyo mmoja wa Wapenzi wa soka ameweza kuonyesha hisia zake kwa MO na hata alipondokewa na Ajibu kwenda Yanga na wachezaji wengine akiwataja  pia ......... Mpenda soka huyo anaeleza kwa machungu jinsi gani anavyomkubali MO na jinsi gani uongozi unavyowatesa mashabiki hao. Hata hivyo inaonyesha habari hizo ni za uongo za MO kwenda Yanga Sc....... Na, BARAKA MBUBA, ........."Nimeona wadau wengi wa SIMBA wakipinga kuondoka kwa "mo"...

MAJIBU YA KAPOMBE KWA ZAKARIA HANS POPE

Image
" Shomari ni muoga tu ... hatuwezi kuvumilia kumlipa bure mshahara ... anatakiwa kucheza sivyo tutamuacha... vipimo vinaonesha mzima ..." Kauli ya mwenyekiti wa usajili Simba SC ndugu Hans Pope juu ya majeraha ya muda mrefu ya beki wa kulia wa timu hiyo Shomari Kapombe. Simba ilimsajili mlinzi huyo toka Azam FC lakini ameshindwa kuichezea timu hiyo kutokana na majeraha ya muda mrefu. Pope amaefanya mahojiano na kituo cha redio cha EFM " kama wanataka kuvunja mkataba wavunje ....mie bado naumwa na daktari kaniambia huenda nitaanza kucheza mzunguko wa pili sasa kama yeye anaongea na vyombo vya habari bila kuniuliza mimi mie sijui hilo . Mie siogopi kucheza... nishacheza sana sasa mtu kusema naogopa kucheza simuelewi" Shomari Kapombe   Beki wa kulia wa Simba SC akijibu tuhuma za Zakaria Hans Pope ! EFM Sports HQ

DALILI ZA BANKA KUTUA YANGA ZA ANZA KUONEKANA

Image
Huku habari zikisema Simba na Yanga zinapigana vikumbo kumuwania Mohammed Issa ‘Banka’, klabu ya mchezaji huyo Mtibwa Sugar imesema ruksa kiungo huyo kuondoka ila afuate masharti. Pamoja na Simba kuhusishwa na mchezaji huyo, kiufundi Yanga ndiyo yenye nafasi kubwa ya kumsajili kiungo huyo kutokana na uhaba wa wachezaji wa aina yake iliyonayo kuliko Simba. Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema; timu yoyoye inayomuhitaji kiungo huyo ifuate taratibu za uhamisho ambazo zinafahamika na wao hawana kinyongo. Mtibwa ni klabu ambayo imekuwa ikitoa wachezaji wengi na wenye vipaji kwenda timu kongwe za Simba na Yanga kwa miaka kadhaa sasa. “Banka ni mchezaji wetu halali, hivyo kama kuna timu inamuhitaji taratibu zinafahamika cha msingi wafuate hizo taratibu na siyo kupitia njia ambazo si halali. Hatuwezi kuzuia riziki yake. “Hata mchezaji mwenyewe anajua mkataba wake unasemaje na sisi na kama akipata timu nini anatakiwa kufanya, hatuna tatizo naye na hata timu inayomuhi...

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF

Image
Mbeya city wakata rufaa bodi ya ligi maamuzi ya mechi yao na Simba SC jumapili ya tarehe 5 November 2017. Rufaa hiyo inaelezea kutoridhishwa na goli walilofungwa dakika ya 7 na Shiza Kichuya. Wanalilalamikia kwamba ni goli la kuotea ! Note Uongozi wa timu ya Mbeya City umeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulalamikika kutotendewa haki katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC. Mbeya City ilichapwa 1-0 Jumapili na Simba, bao pekee la Shiza Ramadhani Kichuya katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema kwamba uchezeshaji wa refa Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Omar Juma wote wa Dodoma na Michael Mkongwa kutoka Njombe haukuwa wa haki kwa mujibu wa sheria 17 za soka. Bin Zubery

MKUMBUSHENI MANARA MPIRA SIO MCHEZO WA MALAIKA

Image
Mkumbusheni Manara, mpira sio mchezo wa Malaika Kalamu ya Ally Kamwe ANAWEZA kuwa sawa kwa staili yake ya ufanyaji kazi. Kama viongozi wa Simba ambao ndio mabosi wake wanaridhishwa naye, mimi ni nani hadi niuponde utendaji wa Haji Manara? Sina tatizo na kazi ya Manara pindi anaposimama na kuizungumza Simba. Tatizo langu linakuja pindi anapojaribu kuufanya mpira wa miguu uwe mchezo wa malaika. Si sawa hili. Kama tukishindwa kumwambia sasa, tutapata shida sana kumweleza baadaye wakati akiwa ameshapata kundi la wafuasi wa kumwamini. Haji anakosea sana kuchanganya mapungufu ya marefa kwenye maamuzi yao na hila za kuiumiza klabu yake. Hivi ni vitu viwili tofauti. Nitakwambia kwanini. Tangu aingie madarakani, Rais wa Fifa, Gianni Infantino, amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuingiza matumizi ya teknolojia kwenye soka kwa ajili ya kusaidia waamuzi. Lakini mwisho wa siku changamoto zimekuwa nyingi kuliko faida. Kwanini? Sababu ni rahisi sana, soka ni mchezo wa binadamu. Udhaifu w...

GOLI LA SIMBA DHIDI MCC NA MAONI YA WADAU NCHINI; UJUMBE KWA MANARA

Image
Nategemea tena kumskia msemaji wa offside fc akiongelea ubovu wa waamuzi wa tz baada ya mbumbumbu fc kufunga goal la kuibia. Nategemea albino atahitisha kikao na waandishi wa habar kuongelea goli walilopewa mikia fc dhidi ya mbeya city hii leo kwenye uwanja wa sokoine jijini mbeya. Sijui waamuz hawa wanatupeleka wap na huu ujinga wao. Kocha wa mbeya city hajaamini kama hawa waamuzi wamekaa darasani kusomea hiyo koz yao maana ni madudu zaid ya madudu kwa soka la tz. Hongereni offside fc kwa kubebwa leo. Haya Sasa We Bwege Leo Chukua Tena Smart Phone Na Tv Uaite Waandishi Wa Habar Uwaoneshe Lile Goli Alilofunga Ashura Kichura Chura Na Umwandikie Barua Waziri Wa Michezo Kwamba Leo Refa Kawabebeni Kwa Kuwapa Goli La Off Abdala Maana Kwenye Offside Ilipitiliza Kabisa ''HAWA VUVUZELA FC BAADA YA KUSHINDA MECHI YA LEO WANAFURAHI NA KUDAI KUWA WANAUWEZO WA KURUKA MAGHOROFA BAADA YA KUTOROKA PORINI, MNAJIDANGANYA WENYEWE TUPO ENDELEENI KUKAIMU CHEO CHETU. MNAJUA ITAKUWAJE SUBIR...

NI LWANDAMINA VS HANS VAN PLUIJM LEO

Image
LWANDAMINA VS HANS VAN PLUIJM JUMAMOSI HII Jumamosi hii wapenzi wa ligi kuu Tanzania bara wanakwenda kushuhudia moja ya mechi yenye gumzo la aina yake ambayo toka kuanza kwa ligi ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa . Hii ni mechi kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya wageni wa ligi Singida United itakayopigwa katika dimba la Namfua mjini Singida baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa wa kupandwa nyasi upya sehemu ya kuchezea . Hans Van Pluijm kocha mkuu wa Singida United kwa mara ya kwanza anakutana katika ligi kuu na timu ambayo kwa nyakati tofauti ameifundisha na kuipa mafanikio makubwa . Hans Van Pluijm mwenye falsafa ya soka la kidachi kushambulia muda wote , aliweza kuipa Yanga vikombe viwili vya ligi kuu Tanzania bara , Ngao ya jamii , Azam Sports Federation Cup na msimu wa 2016 kuwafikisha hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika . Huyu ndie aliyemwachia kijiti George Lwandamina ambaye anaionoa Yanga SC kwa sasa akiwa tayari ameendeleza wimbi la ushindi kwa kuw...