Nategemea tena kumskia msemaji wa offside fc akiongelea ubovu wa waamuzi wa tz baada ya mbumbumbu fc kufunga goal la kuibia. Nategemea albino atahitisha kikao na waandishi wa habar kuongelea goli walilopewa mikia fc dhidi ya mbeya city hii leo kwenye uwanja wa sokoine jijini mbeya. Sijui waamuz hawa wanatupeleka wap na huu ujinga wao. Kocha wa mbeya city hajaamini kama hawa waamuzi wamekaa darasani kusomea hiyo koz yao maana ni madudu zaid ya madudu kwa soka la tz. Hongereni offside fc kwa kubebwa leo.
Haya Sasa We Bwege Leo Chukua Tena Smart Phone Na Tv Uaite Waandishi Wa Habar Uwaoneshe Lile Goli Alilofunga Ashura Kichura Chura Na Umwandikie Barua Waziri Wa Michezo Kwamba Leo Refa Kawabebeni Kwa Kuwapa Goli La Off Abdala Maana Kwenye Offside Ilipitiliza Kabisa
''HAWA VUVUZELA FC BAADA YA KUSHINDA MECHI YA LEO WANAFURAHI NA KUDAI KUWA WANAUWEZO WA KURUKA MAGHOROFA BAADA YA KUTOROKA PORINI, MNAJIDANGANYA WENYEWE TUPO ENDELEENI KUKAIMU CHEO CHETU. MNAJUA ITAKUWAJE SUBIRINI MECHI ZA WEEK END IJAYO MTAELEWA NINACHOMAANISHA. WAKIMATAIFA TUPO
KWA WAKATI MMOJA SIMBA HUCHEZESHA MILIONI ZAIDI YA HAMSINI UWANJANI''.
Na Thadei Ole Mushi.
''Ni kweli kuwa Club ya Simba kwa sasa ndio Club yenye kikosi Ghali kuliko timu nyingine za VPL Tanzania Bara. Jumapili iliyopita nilisema kuwa Value for Money haionekani pale Simba wengi wakanitukana. Kikosi cha simba ni Ghali lakini Si Kikosi Bora.
#Ila bado msimamo wangu upo pale pale, kwa Leo Simba imeshusha kikosi cha Milioni 57 kwenda juu kwenye match ya Leo. Hapa nimechukua tu mishahara ya wachezaji. Chukua mshara wa Niyonzima milioni 8.7, Okwi milioni 7.6, Boko milioni 6.9, Mavugo milioni 4.5, Mkude milion 4.5, Manula Milion 5.1, Shabalala milioni 4.2, Nyoni milioni 5.3, Kichuya milioni 2.4, Mzamiru milioni 2.6 Murshid milioni 5.3 jumla yake unapata milion 57.1 kwa match Moja. Kuna kipindi inazidi hadi kufikia milioni 63 plus kama Mwanjale ataanza.
Kikosi hiki kilisajiliwa kwa lengo kuu moja tu la kuchukua Ubingwa matokeo mengine ya kupendeza yatakayotokea yatakuwa ni manufaa ya ziada.
Cha kushangaza mpaka leo Game ya Tisa bado Simba haijaonyesha viashiria vya Ubingwa. Timu zinazokuwa bingwa katika ligi huwa na Element za Ubingwa kwa kushinda match ngumu na kushinda njee na ndani ya uwanja wao wa Nyumbani. Mpaka sasa kwa jinsi mambo yalivyo Timu yoyote kati ya Simba, Yanga, Azam na Mtibwa wanaweza kuwa bingwa.
#Kama si Refa na refa wa Pembeni kutokuwa makini Leo Simba ingetoka suluhu. Ni aibu kwa club ya Gharama kama Simba kushinda kwa kubebwa na maamuzi mabovu ya Refa.
#Simba ipo kwenye Pressure kubwa kila match utafikiri ndio msimu unamalizika, Bench la Ufundi lina Pressure, Mashabiki wana pressure na wachezaji wana pressure. Hii sio dalili nzuri na kama Simba itapoteza match hata Moja pale Msimbazi kitanuka asubuhi.
#Kwa sasa Kocha anachezesha kikosi cha mashabiki, mchezaji atakaye pigiwa kelele kuwa achezeshwe utamuona match inayofuata. Jambo hili limekuwa likiingilia maswala ya Ufundi ya Banch la ufundi.
#Tuombe Mungu Manula asiumie pamoja na Kichuya. Yaani ili Simba iendelee kushinda hawa watu wawili lazma wawe kwenye afya njema na kwa kiwango kwa asilimia 100. Bila hawa watu wawili hakuna Timu pale''.
Ole Mushi
Edo Kumwembe
''Kamera haionyeshi Kichuya alikuwa wapi wakati mpigaji wa pasi anapiga ule mpira....Siwezi kusema kama ni Offside au sio....sio kila adui anayekuwa mbele ya kipa peke yake anakuwa offside...Kamera hazijatusaidia sana. Thanks..!!!''
Comments
Post a Comment