MANARA AANZA KUWAKERA BAADHI YA WANASIMBA
Soma hapa maoni ya mdau huyu wa simba
Any Way
Wamesema Sana Baada Ya Kupata Ile Droo
Na kashfa Nyingi Bado Zinaendelea Juu Ya Matokeo Ya Tarehe 28/10....
Kwa Kweli Ni Matokeo Mabovu Sana,Tuwe Wakweli Na Tuachane Na Ushabiki Wa Kupenda Penda Hata Kama Tunaona Kabisa Tunakosea Wapi.
Baada Ya Matokeo Yale,Pamekuwa Na Malalamiko Sana Kiasi Kwamba Mpaka Msemaji Wa Simba Ndugu Haji Manara Kuanza Kuweka Preas Conference Na Waandishi Wa Habari.
Kimtazamo Wangu Mimi,Naona Haji Anaongea Sana Na Kutufanya Mashabiki Kuhisi Kuwa Tunaonewa Kwa Kila Kitu.
Kiufupi Timu Ilicheza Chini Ya Kiwango Na Baadhi Ya Wachezaji Wetu Hawaku Perform Kutokana Na Uwezo Wao.Mf:-James Kotei Alivurunda Sana Ile Game,Aliacha Kucheza Mpira Na Akaanza Kumparamia Ajib Tu.
Sikuridhika Na Kiwango Kile,La Pili Tulikuwa Na Uwezo Wa Kumaliza Game Dakika 90 Kwani Wapinzani Wetu Walianza Kwa Kujihami Sana Tu.
Lakini Hatimae Game Ikabadilika Kwa Kukosa Weledi Wa Viungo Wa Kati Na Kumfanya Tilshishimbi Kutawala Duara La Kati Kwa Takriban Dakika 70 Za Mchezo.
Utawala Wa Tshishimbi Uliisha Mara Baada Ya Kuingia Jonas Mkude Ambae Alitawala Vzr Mpaka Mwisho Wa Mchezo.
Mchezo Kwa Kweli Ulikuwa Mgumu Sana Kwetu.
Sasa Huyu Haji Manara Amekuwa Ni Chanzo Cha Kututukanisha Mashabiki Wa Simba Hasa Pale Anapofanya Mikutano Na Kuongea Pumba Zake Za Majigambo Ambayo Baadae Kwa Matokeo Yale Yanawafanya Watani Kutoa Maneno Makali Sana.
Sasa Ninyi Wenzangu Munaonaje Kuhusu Huyu Huyu Msemaji Wetu?
Je Ana Mantiki Ya Kuendelea Kuwa Msemaji Wa Club?
Na Kwa Haya Yanayo Endelea Je Munadhani Anaipeleka Wapi Timu Yetu?
Ni Yeye Ndie Aliyetuamisha Kuwa Kikosi Chetu Kina Thamani Ya 1.3b Yeye Ndio Nayeye Ndie Anaewaamisha Wapenzi Wa Simba Kuwa Tuna Kikosi Imara Chenye Thamani Hiyo.
Cha Kushangaza Timu Imesajili Wachezaji Wazuri Tu Lakini Hawapati Nafasi Ktk Kikosi,Mfano Nicolas Gyan Ambae Alikuwa Ni Top Score Katika Ligi Ya Kwao Ghana,Lakini Kaja Simba Hajapata Hata Nafasi Ya Kucheza Mechi Mbili Mfululizo Kwa Dakika Zote,Tuna ViJana Wengi Sana Ambao Ni Wazuri Kama Jamal Mwambeleko,Yusuf Mlipili,Mohamed Ibrahim Na Wengine Wengi,Nao Bado Kuna Changamoto Ya Kupata Nafasi,Sasa Ina Maana Kocha Kikosi Kimekuwa Kipana Sana Kwake Mpaka Kushindwa Kupata First Eleven Kwa Mechi Ya Tisa Sasa?
Kiukweli Sielewi Kabisa Na Hapo Baadae Tuna Michuano Ya Kimataifa Na Napata Wasiwasi Mkubwa Kama Tunaweza Kuwa Bora Ktk Michuano Hiyo Wakati Ktk Ligi Bado Tunasua Sua.
Haya Ya Kocha Omog Nitakuja Ktk Makala Nyengine Ila Kwa Sasa Tumuangalie Huyu Msemaji Wetu Maana Imekuwa Too Much Sasa Yeye Na Media Kila Kukicha
Naomba Tusaidiane Nini Kifanyike Kwa Msaada Wa Timu Yetu.
Aliandika mdau huyu wa MSIMBAZI
Comments
Post a Comment