Posts

Showing posts from October, 2017

MANARA NA SIMBA YAKE WAANZA KUSHITAKI MAREFA

Image
Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema klabu yake imeandika barua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe kumlalamikia baadhi ya matukio yanayozua utata yanayosababishwa na waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara pindi Simba inapokuwa inacheza na timu nyingine. Manara akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari amethibitisha kwamba, Simba imeandika barua kwenda TFF, Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi na nakala imepelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo (Dkt. Harisson Mwakyembe). “Tumeandika barua TFF, Bodi ya Ligi na nakala tumempelekea Waziri mwenye dhamana ya Michezo na Chama cha Waamuzi, barua itakwenda kulalamikia maamuzi mabovu yanayofanywa na waamuzi wa mpira, sizungumzii Yanga ndio maana nimeweka matukio yote (Mbao na Stand) mechi zote zikiwa mfululizo”-Haji Manara. “Niliwahi kushauri kwa TFF wakae na waamuzi wazungumze nao wawaeleze na sisi hatutaki kubebwa, tunataka ‘fair’ timu ikiwa inastahili kupewa penati dhidi yetu ipewa, tukistahili...

Yanga for life Yafanya kweli kwa wachezaji hawa YANGA

Image
Group la WhatsApp la ‘Yanga for life’, likiwakilishwa na msanii wa filamu nchini, Vicent Kigosi, ‘Ray’, wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘shin gard’, kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi. Straika Ibrahim Ajib, amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili, Kagera na Stand United. Papy Kabamba Tshishimbi, aliyechagulia nyota wa mchezo wa ‘Derby’, dhidi ya Simba, amekabidhiwa Tsh 500, 000 huku kipa Youthe Rostand, akipata Tsh 200,000, viatu na ‘shin gard’. “Tunafanya hivi kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji wetu. Kwa Mwanayanga yeyote atakayependa kujiunga na kundi letu, atutafute kwa namba 0717 554545. Lengo letu ni kuiona timu yetu inafanya vizuri na kutwaa ubingwa mara nne mfululizo,” alisema Ray.

Michuano ya CECAFA kuanza kutimua vumbi Novemba 25

Image
Michuano ya CECAFA kuanza kutimua vumbi Novemba 25. Mashindano ya kombe la Afrika Mahariki na Kati (CECAFA) yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 9 mwaka huu, huku timu za Zimbabwe na Libya zimealikwa kama wageni kushiriki. Mashindano haya hayakuandaliwa mwaka jana baada ya wenyeji Sudan kujiondoa na kisha Kenya iliyochukua nafasi ya kuandaa nayo kujiondoa dakika za mwisho.  Nchi zitakazoshiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Sudan kusini, Djibouti, Eritrea, Somalia na Zanzibar. na samuel samuel

Kumwembe vs Manara

Image
Sikiliza...1-1 Taifa....lakini, Yanga haikuwa na Three key players..Kamusoko, Ngoma na, Tambwe. Na walikosa mabao ya wazi zaidi. Something is missing Msimbazi. Wachezaji hawana authority kubwa uwanjani kama ambavyo rafiki yangu Haji Manara na mashabiki wanataka. Kama unaweza kusema Simba ina Wacheza wengi wapya na inahitaji muda basi hata Yanga leo ilikuwa na wachezaji wapya nusu ya timu. Raphael, Buswita, Gadiel, Ajib, Rostande, Tshishimbi..game pekee ambayo Simb walionyesha authority kubwa uwanjani (kwa mtazamo wangu) ilikuwa dhidi ya Mbao away...Kuna kitu hakifikii matazamio pale Msimbazi. Kama sio wachezaji kujua uzito wa jezi wanayovaa, basi Labda benchi la ufundi kuna tatizo. Anyway, na nyinyi Yanga hivi Kichuya amewakodi?

TATHIMINI YA SIMBA VS YANGA ILOPIGWA JANA

Image
TATHIMINI YA KARIAKOO DERBY Na Samuel Samuel Mtanange wa watani wa jadi kati ya Yanga SC na Simba SC almaarufu kama Kariakoo derby umemaliza uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kwa timu zote kutoshana nguvu kwa sare ya 1-1. Alikuwa mnyama Simba SC aliyekuwa wa kwanza kuwanyanyua maelefu ya mashabiki wake vitini kupitia kwa Shiza. Kichuya baada ya kuicheza vyema krosi ya Emanuel Okwi. Hii ilikuwa dakika ya 57 baada ya timu zote kwenda mapumziko zikiwa suluhu bin suluhu. Dakika tatu baadae Yanga waliweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wao wa kati Obrey Chirwa na mwisho wa mchezo matokeo kusomeka 1-1. *TATHIMINI* Tukianza na wenyeji wa mchezo Yanga SC; waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-4-2 . Ukuta wa nyuma ukiwa na walinzi wanne Juma Abdul kulia na Gadiel Mbaga kushoto wakicheza kama walinzi wa pembeni. Kati walisimama Andrew Vicent na nahodha Kelvin Yondani. Eneo la kati ; Pappy Tshishimbi kama kiungo mkabaji ambaye alikuwa akicheza kama box to box m...

TIKETI ZA SIMBA VS YANGA ZA TISHIA WENGI KUIKOSA MECHI HIYO LIVE

Mashabiki wa Simba na Yanga wana hofu kubwa ya kuukosa mchezo kati yao utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru. Hofu ya kuukosa mchezo huo unatokana na idadi ndogo ya watazamaji 23,000 tu watakaoingia kwenye Uwanja wa Uhuru wakati ilizoeleka watu 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kiiingilio ni Sh 10,000 kwa mzunguko na 20,000 kwa jukwaa kubwa. Lakini inaonekana mapema lazima kutakuwa na suala la ulanguzi. Inawezekana kabisa wako watakaonunua tiketi mapema na kuanza kuziuaza kwa bei kubwa. Lakini kama zitakatwa getini siku ya mechi, pia inaweza kusababisha vurugu kwa kuwa watu hawatakuwa na uhakika na inawezekana idadi kubwa ikakosa hivyo kusababisha tafrani. Watu wengi waliochangia kwenye mtandao wa SALEHJEMBE wanaonekana kuwa na hofu ya kukosa tiketi na wanahofia ulanguzi.

Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi. MAYAI Ndani

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi. Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ambayo ataiongoza yeye mwenyewe ni Shani Mligo (Makamu Mwenyekiti), Boniface Wambura (Katibu), Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa. Wengine ni Dr Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay. Kamati hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL). Pia Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa (Majeki). Kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji (Governing Regulations) za TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi. Boniface Wambura Ofisa Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi Kuu Ta...

KUELEKEA KARIAKOO DERBY

Image
KUELEKEA KARIAKOO DERBY Aishi Manula vs Youthe Rostand Walinda mlango hawa mahiri bila shaka ndio watakao simama langoni mwa timu zao siku ya jumamosi kwenye mtanange wa watani wa jadi kati ya Simba SC na Yanga SC uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Aishi Manula akisimama kama golikipa namba moja wa Simba SC ambaye amecheza mechi zote saba mpaka sasa akiruhusu nyavu zake kutikisika mara 4 . Youthe Rostand ni kwa upande wa Yanga SC ambaye pia amekaa langoni katika mechi zote 7 za Yanga msimu huu akiruhusu lango lange kutikiswa mara 3 tofauti ya goli 1 kwa Aishi Manula . Manula Ndio tegemeo la Simba langoni akiwa na akili kubwa kuwapanga walinzi wake pia akiwa na kipaji kikubwa kwenye saving, positioning pia kutoa ushauri kwenye marking kutokana na kuiona timu tokea nyuma. Ana tuzo ya kipa bora wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mfululizo jambo ambalo linaakisi uwezo wake . Cha ziada kwake ni uwezo wa kucheza penati na kujiamini langoni. Mapungufu yake... Pressing inapok...
Image
Baraka Adson Mpenja  : Ajibuuuuuuuuuuuu.......... ...... " tuwe na kiasi katika mapenzi ya soka. Jiandae vyema kisaikolojia kupokea matokeo ya aina yoyote ya timu yako. Wengi wamepoteza maisha au kupata matatizo makubwa kiafya kisa ushabiki tu wa mpira . Ni vyema kuipenda timu yako lakini mapenzi yenye gharama ya uhai tumpe Mungu kwanza ! "  " ushawahi kukosa misa msikitini au kanisani ukazimia kwa hofu ya kumkosea Mungu namna hii? 👇🏽 au kutenda maovu ukawa na hofu kuu kama uliyonayo hivi sasa kuelekea mechi hii?! Hapana tuikatae hali hii kwa nguvu zote "  Samuel USHAURI WA BURE Kesho kila mmoja wetu awe shabiki wa simba au yanga ajiandae kisaikolojia kwa matokeo ya aina yoyote ile. hii ni katika kujiweka sawa kujiepsha na mshituko pindi timu yako itakapopata matokeo kinyume na matarajio.

VITA YA WACHEZAJI YA YANGA NA SIMBA 28/10/2017 NI AJIBU AU OKWI?

Image
KUTOKANA na viwango vya soka vilivyoonyeshwa na Yanga, Simba  kwenye mechi zao mwishoni mwa wiki iliyopita pamoja na takwimu walizokusanya baada ya mechi saba za Ligi Kuu Tanzania Bara, inatoa picha halisi ya upinzani utakaokuwapo kwenye mtanange wa watani hao wa jadi utakaopigwa Jumamosi hii. Kwa sasa Simba ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania, wako moto na Yanga wanaoshika nafasi ya pili pia ni moto, ambapo kwa watoto wa mjini wanasema ugali moto na mboga moto. Mpaka sasa mechi hiyo haijajulikana itachezwa wapi, ingawa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeonyesha kuwa mchezo huo unaweza kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Lakini kutokana na mchezo huo wa Yanga na Simba kuwa ni moja ya ‘derby’ kubwa barani Afrika, ukiziacha zile za Orlando Pirates na Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), Raja Casablanca vs Wydad Athletic Club (Morocco), Al Ahly vs Zamalek (Misri), Club Africain vs Esperance Sportive de Tunis (Tunisia),  bila shaka Serikali inawez...

KUELEKEA KARIAKOO DERBY YANGA NA SIMBA

Image
KUELEKEA KARIAKOO DERBY........ YANGA SC Huu ni mwendelezo wa makala ya awali juu ya joto la mechi ya watani wa jadi jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Baada ya kuitazama Simba SC kiundani sasa tuwaangazie mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara ambao ndio watakuwa wenyeji wa mechi hiyo dhidi ya mahasimu wao Simba SC. Kama ilivyo Simba, Yanga pia wanaingia katika mechi hii wakiwa na mtaji mzuri kisaikolojia , kimbinu , kiufundi, ari ya kupambana na hamasa kubwa ya kulinda heshima yao ya soka nchini kama mabingwa mara tatu mfululizo pia wakitaka uongozi wa ligi baada ya kulingana pointi sawa na Simba lakini Simba wakiongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga . LWANDAMINA Huyu ndio kocha mkuu wa Yanga ambaye anaingia kwenye mtanange huu akiwa na pressure kubwa kushinda mechi ya derby baada ya kucheza mechi tatu na kuambulia patupu baada ya kufungwa mechi tatu. Lwandamina msimu wa 2016-17 alianza na kupoteza 2-1 na Simba SC. Kwenye michuano ya Mapindu...

YANGA IMEKUWA NA JICHO LA MWEWE KWA SIMBA SC

Image
YANGA IMEKUWA NA JICHO LA MWEWE KWA SIMBA SC Anaandika mchambuzi Samuel Samuel 1997 Simba SC walishindwa kuzuia uhamisho wa Akida Makunda kwenda Yanga ambaye baadae aligeuka mwiba mkali kwa klabu hiyo na pia kusimama kama nguzo muhimu kwa Yanga safu ya kiungo na washambuliaji wa pembeni. Uhamisho wa kaka yangu huyu ni moja ya uhamisho unaosimama mpaka leo kama uhamisho wa uchungu sana kutokana na kiwango alichokuanacho Akida. 2007 Idd Athuman ' Chuji ' moja ya viungo bora kuwahi kucheza ligi kuu Tanzania bara . Alitua Simba SC mwaka 2006 akikutana na vijana wenzake wa miaka hiyo Henry Joseph , Kelvin Yondani na Victor Costa . Hakika walikuwa muhimili imara wa Simba SC kwenye kiungo na ulinzi bila kumsahau Ko'koo. Simba wakavurugana na Chuji . Kijana akafikia kusema ' kubaki Simba ni bora niuze ndimu ' . Yanga msimu wa 2007 wakamnyakua . Ubora wa Chuji Yanga na timu ya taifa ambao mpaka sasa hakuna aliyethubutu kuusogelea uliendelea kubakia jinamizi la mat...

Who will finish the season as the top goalscorer in the English top flight?

Image
Who will finish the season as the top goalscorer in the English top flight? we bring you  you the latest in the race for the Golden Boot The race for the 2017-18 Premier League Golden Boot is well and truly on, with the usual suspects surging into an early lead. Harry Kane was the clear winner of last season's crown, bagging 29 goals in 30 appearances for Tottenham, while Romelu Lukaku followed with 25 in 37 games for Everton. New faces such as Chelsea forward Alvaro Morata and Arsenal striker Alexandre Lacazette have been added into the mix this season, meaning that the competition is certainly greater. And the battle is currently as tight as expected, with Kane just edging out Lukaku and Sergio Aguero following the ninth matchday of the season. Premier League top goalscorers: *Correct as of games on October 22, 2017 Pos Player Club Goals =1 Harry Kane Tottenham 8 =2 Romelu Lukaku Manchester United 7 =2 Sergio Aguero Manchester City 7 =4 Alvaro Morata Chelse...

AJIBU WA YANGA DAH! KOMBINESHENI YAKE NA CHIRWA NI MOTO WA KUOTEA MBALI

Image
Ajibu wa YANGA ndivyo unavyoweza kusema.  mchezaji mahili wa timu ya dar young africa maarufu kama YANGA leo amezidi kudhihirisha kuwa yeye ni moto wa kuotea mbali hasa baada ya kuonesha kiwango bora zaidi katika kila mechi aliyo kichezea kikosi cha wanajangwani hao. Ajibu ameweza kufunga magori mengi ambayo huwa yanawainua wapenzi wote wa soka nchini. Ajibu ibra kadabla migomba au miguu ya zahabu huzikonga nyoyo za wapenzi wa soka nchini si kwa kufunga tu magori au kutoa pasi safi bali hata staili yake ya uchezaji chenga n.k.  ajibu hana mpinzani sasa nchini kutokana kua na aina ya peke yake ya kuli sakata gozi la ng'ombe awapo uwanjani kwani huleta burudani hakika. Muunganiko wake na Obrey Chola Chirwa raia wa zambia hakika ina onekana kuwa bora kila kukicha , katika mechi mbili za mwisho wamelidhihirisha hilo kwa kutengenezeana pasi za Magori kila wapatapo nafasi na kufunga. Hakika wameonesha uelewano mzuri sana wachezaji hawa na kuweza kuifanya yanga kuonesha ubora wa...

YANGA YAMSHITUKIA OMOG KWA MATOKEO HAYA

Image
NI KAMA OMOG ANATUMA SALAMU JANGWANI Ukiondoa kiwango kibovu cha Mji Njombe hususani eneo lao la ulinzi na wing yao ya kushoto, bado vijana wa msimbazi leo walikuwa katika kiwango bora kuliko hata kwenye ushidi wa goli 7 dhidi ya Ruvu shooting mechi ya ufunguzi. Omog ameingia uwanjani leo kuonesha makucha halisi ya Simba SC ligi kuu kwa uwezo wake kurarua kila aliye mbele yake katika mtindo ambao yeye anaamua. Mara waalimu wa timu kubwa wanapokutana na timu ndogo ( underdogs ) hujiandaa katika hesabu za kukamiwa hivyo hujiweka imara eneo la kiungo cha kati mathalani kwa kutumia viungo wakabaji wawili au watatu pia walinzi imara wanaoweza ' battling ' kwa maana ya matumizi ya nguvu kwenye counter na one against one.  Kwa msingi huo wengi walitarajia Omog angeanza na Jonasi Mkude chini akicheza sambamba na James Kotei kutengeneza ' double six ' ambayo ingekuwa inazungukwa na holding midfielder Niyonzima akicheza huru au Okwi akicheza chini sana kama ' deep pla...

ABDI BANDA AZIDI KUAMINIWA BAROKA FC SAUZ

Image
Timu ya Abdi Banda ligi kuu nchini Afrika Kusini, Baroka FC walazamishwa sare na Golden Arrows . Banda ameendelea kutumika kikosi cha kwanza toka atue timu hiyo mapema mwanzoni mwa msimu huu. Baroka walipata goli mapema dakika ya 15 kupitia kwa Moeti lakini Golden Arrows walichomoa dakika ya 75 kupitia Magubane. Vikosi vyote vilikuwa hivi; Baroka FC: Vries, Mothupa, Shaku, Mdatsane, Masenamela, Banda, Madubanya, Moeti (Kgaswane 68’), Matloga (Sidumo 82’), Motupa, Macha (Nguzana 60’) Golden Arrows: Gumede, Dube, Mzava, Mngwengwe, Nkombelo, Bilankulu (Shongwe 58’), Cele, Magubane, Mahachi (Mutizwa 71’) , Jooste (Jappie 58’), Lamola @ SAMUEL SAMUEL Hata ivyo wadau na wapenzi wa soka nchini wanaombwa kuwaunga mkono vijana wenye vipaji vya kucheza soka kwa hali na mali ili kuwasaidia wapate nafasi ya kucheza soka la kulipwa ili kuisaidia timu ya taifa ya tanzania kimataifa. Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji vya kulisakata soka ila moja ya changamoto ni uchache wa mawak...

MASIKINI SIMBA

Image
Masikini Simba SC kila jitihada wakiweka mwisho au katikati ya safari mkosi huwakumba....watatoboa safari hii ligi kuu kwa dalili hizi za mapema? Tetesi zilianza za kuondoka Omog, jana afisa habari wa timu hiyo kakanusha ingawa tayari wapenzi na wanachama baadhi wa timu hiyo kukosa imani nae. Asubuhi ya leo gazeti maarufu la michezo nchini Mwanaspoti limeripoti kwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Jackson Mayanja kuvunja mkataba wake na timu hiyo na kumwacha bosi wake Omog. Ukiondoa hayo , bado timu hiyo imeanza kukumbana na adha ya majeruhi kwa wachezaji wake; Kipa Nduda , mshambuliaji John Bocco , mlinzi Shomari Kapombe ambaye toka asajiliwe hajacheza kutokana na majeruhi . Wa nne ni beki wa kutumainiwa Salumu Mbonde. AMEANDIKA Samel samuel Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba na krejea kwao Uganda. Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi. kwa upande wake kocha huyo msaidizi amesema haya...