YANGA YAMSHITUKIA OMOG KWA MATOKEO HAYA
NI KAMA OMOG ANATUMA SALAMU JANGWANI
Ukiondoa kiwango kibovu cha Mji Njombe hususani eneo lao la ulinzi na wing yao ya kushoto, bado vijana wa msimbazi leo walikuwa katika kiwango bora kuliko hata kwenye ushidi wa goli 7 dhidi ya Ruvu shooting mechi ya ufunguzi.
Omog ameingia uwanjani leo kuonesha makucha halisi ya Simba SC ligi kuu kwa uwezo wake kurarua kila aliye mbele yake katika mtindo ambao yeye anaamua.
Mara waalimu wa timu kubwa wanapokutana na timu ndogo ( underdogs ) hujiandaa katika hesabu za kukamiwa hivyo hujiweka imara eneo la kiungo cha kati mathalani kwa kutumia viungo wakabaji wawili au watatu pia walinzi imara wanaoweza ' battling ' kwa maana ya matumizi ya nguvu kwenye counter na one against one. Kwa msingi huo wengi walitarajia Omog angeanza na Jonasi Mkude chini akicheza sambamba na James Kotei kutengeneza ' double six ' ambayo ingekuwa inazungukwa na holding midfielder Niyonzima akicheza huru au Okwi akicheza chini sana kama ' deep playmaker ' na mbele akibaki mshambuliaji wa kati mmoja kama ' lone striker '.
Lakini Omog ameipanga timu kuonesha uwezo wa Simba idara zote ; uwezo katika kujilinda , kutengeneza mashambulizi na kushambulia. Ni mchezo ambao kwa hakika dakika 75 za awali ilionesha ni timu ambayo inacheza soka la kitabuni kujiandaa na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika pia ikionesha ni timu inayojipanga kushinda kila mchezo ulio mbele yake.
Mabadiliko ya kuwatumia Juuko Murshi na Mlipili kama walinzi wa kati limeonesha uhai mkubwa hususani katika utulivu wao kucheza kama walinzi pia viungo wakabaji wa akiba katika kuanzisha mashambulizi hali iliyowafanya Njombe Mji kucheza mbali zaidi ya eneo la Simba SC . Kazi imekuwa rahisi kwao kutokana na classy players kulia na kushoto kwao. Beki ya kulia Erasto Nyoni ambaye amegeuka mwiba mchungu kwa wing ya kushoto ya Njombe kutokana na uwezo wake wa kupanda na kushuka kusaidia mashambulizi na kuimarisha ulinzi . Akicheza chini ya mstari alikuwa ' full back ' lakini akiwa na mpira alikuwa akipanda juu kama kiungo wa pembeni kitu ambacho kiliwawezesha yeye na Kichuya kuwa na marking kubwa kwenye wing na pressing yenye faida. Sanjari kwa Zimbwe Jr kushoto ambaye alilinda vyema safu hiyo na kumpa back nzuri Niyonzima aliyekuwa anacheza huru kwa maana ya kuhama kutoka box moja kwenda jingine au wing moja kwenda nyingine . Silaha kubwa ni jinsi safu hiyo ya ulinzi ilivyokuwa inatuliza mpira na kuanzisha mashambulizi aidha kati au pembeni .
Kiungo cha Simba leo kimeonesha uwezo mkubwa na kutoa onyo kwa timu zinazokuja mbele yake . Omog akitumia mfumo wa 4-3-3 akikipanga kiungo chake katika mfumo wa almasi ( ♦️ ), Jonasi Mkude alicheza kama kiungo mkabaji kulia kwake Shiza Kichuya na kushoto Haruna Niyonzima , juu akifunga Mzamiru Yassin kuunda umbo hilo hii ni katika tactical deployment lakini kiuchezaji ndipo hesabu za Omog zilipoonekana na kuwazidi Njombe .
Mzamiru ambaye alipangwa kucheza kama kiungo mchezeshaji, alisimama kama kiungo mshambuliaji kificho ( invisible attacking midfielder ) na Haruna aliyepangwa wing ya kushoto kama kiungo mshambuliaji ndio alikuwa huru kucheza kama kiungo mchezeshaji ili Mzamiru aweze kucheza second balls zote ambazo Njombe walikuwa wanatengeza kwenye 18 yao au kumalizia mipango ya counter ya haraka ambayo Simba walikuwa wanaisuka kupitia pembeni hususani wing ya kulia. Hili liliwachanganya Njombe ambao walijizatiti kati (defensively) kulinda mfumo ilihali Simba walikuwa wana uwezo mkubwa kufunguka pande kwa uwezo wa kiungo chao.
Ni mfumo ambao umemfanya Mzamiru kuonesha uwezo wake pia kurejea katika kiwango chake cha msimu uliopita . Ni mfumo ambao upo flexible kucheza na timu yoyote inayofunga njia au kufunguka kushambulia. Kwa sababu unaruhusu aina nyingi za uchezaji aidha kuweka pasi chini au kutumia mipira mirefu kutokea pembeni , kikubwa ni uwezo wa wachezaji kwenye uwezo wa kunyumbuka na mfumo.
Mfumo na mbinu hizi unawalazimisha wapinzani kurudi nyuma kujilinda endapo kama hawana kiungo imara kuvunja mipango ya hiyo ' diamond midfield ' na kukataa full backs kupanda juu free. Ukipiga hesabu za haraka kwa aina ya wachezaji ulionao unaweza kuja na 4-2-3-1 ukitumia viungo wakabaji wawili kitu ambacho kama timu haina mawinga wazuri mnaweza kujikuta mmepaki basi mwanzo mwisho lakini timu nyingi Ulaya hupambana pia kwa 4-3-3 ukitumia wachezaji wenye kasi , nguvu na uwezo wa kupambana kuufinya uwanja ili kiungo cha timu pinzi kisitanuke na kujikuta kikicheza flat kuua umbo lake la almasi .
Yanga wanahitajika kujipanga vyema kwenye wings zao , kiungo na walinzi wa kati ili pressing hii ya Simba isiwarudishe nyuma tactically imbalance na kujikuta wanatengeneza mashimo mengi ya akina Okwi na Mzamiru kufunga . Njia nzuri ya kumzuia adui ni kumshambulia.
Ni approach ambayo Omog akiwazoesha vyema vijana wake na wakamuelewa, hakika mnyama anaweza kung'ara msimu huu.
SAMUEL SAMUEL
Comments
Post a Comment