PIGO: SIMBA KWAKOSA WATATU DHIDI YA YANGA

 TIMU ya Simba itawakosa nyota wake watatu kwenye mchezo wa kukata na shoka dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga baada ya taarifa ya daktari kuwataka kukaa nje kwa vipindi tofauti wakiuguza majeraha yao.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita makao makuu ya klabu hiyo, msemaji Haji Manara amesema John Bocco na Salim Mbonde wanaungana na majeruhi wengine Shomari Kapombe na Said Mohamed ‘Ndunda’ na kufanya idadi ya nyota walio nje kufikia wanne huku Bocco pekee akiwa ndiye mwenye uhakika wa kuwavaa Yanga.
“Bocco atakosa mchezo mmoja tu dhidi ya Njombe Mji, lakini Mbonde yeye atakosa michezo minne (Njombe Mji, Yanga, Mbeya City na Prisons) kabla hajarejea uwanjani.
“Madaktari wameshauri Kapombe aendelee kukaa nje ya uwanja hadi atakapopona kabisa huku wao wakiendelea kumwangalia kwa ukaribu,” alisema Manara.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Nduda aliyerejea hivi karibu akitokea nchini India alikofanyiwa upasuaji Manara alisema yeye atakaa nje kwa muda wa wiki nane huku taarifa za kiuchunguzi zikidai Simba inaweza kumkosa Kapombe katika mzunguko wote wa kwanza.
Simba itapambana na Yanga Agosti 28 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa nane siku ambayo Mbonde, Kapombe na Nduda watakuwa hawajarejea uwanjani.

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF