MKWASA ANENA HABARI NJEMA KWA YANGA
KATIBU Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa ameweka wazi kuwa wanapanga kujiimarisha katika masuala ya utawala, usajili na fedha ili kuona timu yao inafanya vizuri katika ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa.
Amesisitiza kwamba hesabu zao ni za mbali sana na wana vikao vya mara kwa mara kuangalia nini cha kufanya huku akiwataka wadau wa klabu kutokuwa na presha kabisa.
“Katika usajili kuna maeneo ambayo mwalimu amepanga kuyaimarisha hivyo tutampa sapoti kubwa. Nafasi ya mchezaji wa kigeni ni moja, ila tutasikiliza mapendekezo ya mwalimu,” alisema Mkwasa, ambaye amewahi pia kuinoa timu hiyo.
Alisema kwamba usajili wao wa dirisha dogo hauangalii majina bali aina ya watu ambao, wakiingia katika kikosi cha Jangwani watawapa pointi tatu ndani na nje ya nchi.
“Tumekuwa na majeruhi wengi sana na tunaangalia namna ya kuwasaidia wachezaji wetu warejee uwanjani kwa haraka, tunahitaji kuwa na timu nzuri.
“Katika masuala ya fedha bado tunatafuta udhamini mwingine. Yanga ni timu kubwa na ina matumizi makubwa ya fedha hivyo tunahitaji kupata hela zaidi. Tunazungumza na baadhi ya kampuni kuona kama wanaweza kutusaidia,” alisema
Comments
Post a Comment