Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi. MAYAI Ndani

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi.
Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ambayo ataiongoza yeye mwenyewe ni Shani Mligo (Makamu Mwenyekiti), Boniface Wambura (Katibu), Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa.
Wengine ni Dr Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay.
Kamati hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL).
Pia Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa (Majeki).
Kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji (Governing Regulations) za TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi.
Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF