YANGA KAMILI KUIVAA KAGERA SUGAR, KUANZA SAFARI KESHO

Klabu ya Yanga leo imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam kujiandaa na mchezo wa raundi ya 6 dhidi ya Kagera  Sugar utakaopigwa Oktoba 14 Kaitaba Stadium Bukoba Mkoani Kagera.

Hofu imepungua kama siKuisha kabisa mara baada ya wachezaji Obrey Chirwa na Amis Tambwe kuonekana katika mazoezi na siyo mazoezi tu mazoezi ya pamoja.

Toka Tambwe amerejea katika mazoezi baada ya Kupona  amekuwa akionekana katika mazoezi  mepesi na Gym lakini leo amefanya mazoezi ya Pamoja hali inayoashiria kuwa yuko fiti kwa asilimia mia moja kuelekea Mchezo ujao dhidi ya KAGERA SUGAR.

Hofu Ilikuwa kubwa mara baada ya Tambwe kutoonekana katika kikosi cha Yanga kilichoshuka dimbani dhidi ya KMC watu wakijua bado Anaumwa na huenda ataukosa Mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Kurejea kwa Tambwe   kutaongeza imani kwenye safu ya Ushambuliaji kwani amekuwa tegemeo kwa UPACHIKAJI wa Mabao katika misimu karibia yote akiwa na Wana Jangwani Yanga. Endelea kufatilia habari za uhakika hapahapa

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF