Mh. MAGUFURI AFANYA HAYA
Rais Magufuli amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na pia amemteua Katibu mpya wa Bunge.
Rais Magufuli ameongeza wizara kutoka 19 hadi 21.
Waziri wa Mazingira January Makamba, Naibu atakuwa Mh. Kangi Lugola
Mbunge George Mkuchika ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora.
Mbunge Luhaga Mpina ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Abdallah Ulega ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo.
Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuwa chini ya Waziri Dr Philip Mpango na Naibu Waziri Dr Ashatu Kijaji.
Wizara ya Kilimo Waziri ni Charles John Tzeba, na Naibu Waziri ni Marry Mwanjelwa.
Selemani Jaffo amepandishwa na kuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, kabla alikuwa Naibu kwenye Wizara hiyo.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zimekuwa Wizara mbili za Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi:
Wizara ya Habari utamaduni wasanii na Michezo, Waziri ni Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri ni Juliana Shonza.
Wizara ya Madini, Waziri ni Angela Kairuki na Naibu Waziri Harun S Nyongo.
Wizara ya Nishati, Waziri atakuwa Medadi Kalemani Naibu Waziri Subira Hamisi.
Katibu wa bunge Steven Kagaigai na Dkt. Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.
Comments
Post a Comment