Yanga for life Yafanya kweli kwa wachezaji hawa YANGA


Group la WhatsApp la ‘Yanga for life’, likiwakilishwa na msanii wa filamu nchini, Vicent Kigosi, ‘Ray’, wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘shin gard’, kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi.
Straika Ibrahim Ajib, amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili, Kagera na Stand United.
Papy Kabamba Tshishimbi, aliyechagulia nyota wa mchezo wa ‘Derby’, dhidi ya Simba, amekabidhiwa Tsh 500, 000 huku kipa Youthe Rostand, akipata Tsh 200,000, viatu na ‘shin gard’.
“Tunafanya hivi kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji wetu. Kwa Mwanayanga yeyote atakayependa kujiunga na kundi letu, atutafute kwa namba 0717 554545. Lengo letu ni kuiona timu yetu inafanya vizuri na kutwaa ubingwa mara nne mfululizo,” alisema Ray.


Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF