KUELEKEA KARIAKOO DERBY
KUELEKEA KARIAKOO DERBY
Aishi Manula vs Youthe Rostand
Walinda mlango hawa mahiri bila shaka ndio watakao simama langoni mwa timu zao siku ya jumamosi kwenye mtanange wa watani wa jadi kati ya Simba SC na Yanga SC uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Aishi Manula akisimama kama golikipa namba moja wa Simba SC ambaye amecheza mechi zote saba mpaka sasa akiruhusu nyavu zake kutikisika mara 4 . Youthe Rostand ni kwa upande wa Yanga SC ambaye pia amekaa langoni katika mechi zote 7 za Yanga msimu huu akiruhusu lango lange kutikiswa mara 3 tofauti ya goli 1 kwa Aishi Manula .
Manula
Ndio tegemeo la Simba langoni akiwa na akili kubwa kuwapanga walinzi wake pia akiwa na kipaji kikubwa kwenye saving, positioning pia kutoa ushauri kwenye marking kutokana na kuiona timu tokea nyuma. Ana tuzo ya kipa bora wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mfululizo jambo ambalo linaakisi uwezo wake . Cha ziada kwake ni uwezo wa kucheza penati na kujiamini langoni.
Mapungufu yake...
Pressing inapokuwa kubwa hupoteza utulivu langoni . Magoli mengi amefungwa kutokana na hilo. One against one na pressure kubwa ndani ya 18 humfanya kutokana katika muhimili wake lakini pia si mzuri sana kwenye michomo ya kona kutokana na kimo chake. Mechi na Mtibwa alifungwa goli la kona.
Youthe Rostand
Kama ilivyo kwa Manula , huyu pia ni mlinda mlango namba moja kwa Yanga hivi sasa aliesajiliwa msimu huu tokea African Lyon. Ana uwezo mzuri langoni hususani kutumia kimo chake kirefu na umbo kubwa kucheza mipira ya juu ( aerial balls ) , smart in saving, punching and positioning. Ni mzuri kuwapanga mabeki wake kwenye set pieces lakini pia ameonesha uwezo mzuri kwenye one against one .
Mapungufu yake...
Si mzuri katika hesabu za kutoka golini hususani kwa washambuliaji wanaosogea kwa kasi langoni kwa ajili ya kuinua mipira juu ( parabolic). Mechi na Kagera aliruhusu goli kutokana na kukosa hesabu nzuri na walinzi wake kabla ya kutoka .
Jumla
Aishi Manula na Youthe kwa pamoja bado ni imara sana kulinda milango yao dhidi ya washambuliaji wa timu zote mbili . Udhaifu wao unazibwa vyema na walinzi endapo mwalimu atakuwa ameiandaa timu vizuri kwenye defensive patterns.
Manula ; kuondoa pressure kwenye 18 yake na kutoruhusu one against one ni uimara wa viungo wa kati na walinzi wa kati kumfanyia shielding lakini pia mfumo wa kukabia juu ni mzuri kwake ili awe huru kutazama movements za mpira tokea mbali. Tishio kubwa kwake ni uwezo wa Ibrahim Ajibu wa Yanga SC ambaye hupangwa kama kiungo mshambuliaji na mshambuliaji. Huyu kutokana na uwezo mkubwa kukokota mipira kwa kasi kuelekea kwenye attacking zone ( D ), huruhusu pressure kwa viungo wa chini na walinzi wa kati ambao hurudi nyuma wakiwa hawana utayari mzuri wa kujipanga kuzuia . Endapo viungo wa Simba na walinzi wao wakimwacha huru Ajibu au wakijisahau katika hilo basi Manula atakuwa katika hali ngumu kumkataa Ajibu ambaye anaweza kufunga au kuwafanyia screening wenzake ndani ya 18. Sanjari na hilo ni mpiga namba moja wa kona na faulo za Yanga zenye madhara .
Rostand; Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kufunga nje ya 18. Emanuel Okwi huyu anaweza kuyatumia makosa ya Rostand katika kutoka langoni , Okwi ana uwezo mzuri wa kukaa na mpira pia kufunga kwa kunyanyua mipira juu ( volleys ) . Endapo walinzi wa kati wa Yanga watamwacha aingie huru ndani ya tatu yao anaweza kumwadhibu. Saidi Ndemla huyu ni mtaalamu kwenye ' faking ' anaweza kuwa na mpira nje ya mita 40 au 30 akasogea kama bado anaendelea kuchezesha timu au kutazama nafasi ya kupiga final pass lakini akakunjuka na thunderbolt kutokana na jinsi ya kipa alivyoshindwa kupunguza goli na viungo au walinzi kuziba njia . Mzamiru Yassin pia Shiza Kichuya wana uwezo wa kupiga mashuti ya haraka tokea pembeni kama counter. Rostand inampasa kuwa makini sana kwenye kutoka pia walinzi wake kuwa wepesi kwenye blocking and clearance na kuicheza vyema mipira ya juu ili kutoruhusu ' free header ' kwa Okwi au Mavugo ambao ni wazuri wa kutumia fursa hizo.
SAMUEL SAMUEL
USIKOSE MAKALA IJAYO
Comments
Post a Comment