INIESTA APIWA PINGU BARCELONA
ANDRES INIESTA AJITIA KITANZI CHA MAISHA NA FC BARCELONA
Andres Iniesta amesaini mkataba utakao muweka Barcelona maisha yake yote.
Klabu ya Barcelona imetangaza mkataba wake mpya na kiungo huyo kama ' deal for life ".
Iniesta mwenye miaka 33 ameshinda vikombe 8 vya La liga na miamba hiyo ya soka na mara 4 kombe la klabu bingwa Ulaya. Pia ameshinda Europa mara mbili huku akiwa na medali ya dhahabu ya kombe la dunia na timu yake ya taifa ya Uhispania.
Iniesta anashika rekodi ya pili katika klabu hiyo kwa kucheza mara nyingi zaidi . Ameichezea klabu hiyo mara 639. Xaiv anaongoza kuichezea klabu hiyo mara nyingi zaidi baada ya kuichezea timu hiyo mara 767
Andres bado yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania licha ya kutoichezea timu hiyo kwa sasa kutokana na majeruhi. Ameichezea timu hiyo mara 121 na kuifungia mara 13.
Anakumbukwa sana katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010 Uhispania wakicheza fainali na Uholanzi alifunga goli la ushindi Uhispania wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa 1-0 nchini Afrika kusini.
Comments
Post a Comment