MASIKINI SIMBA

Masikini Simba SC kila jitihada wakiweka mwisho au katikati ya safari mkosi huwakumba....watatoboa safari hii ligi kuu kwa dalili hizi za mapema?
Tetesi zilianza za kuondoka Omog, jana afisa habari wa timu hiyo kakanusha ingawa tayari wapenzi na wanachama baadhi wa timu hiyo kukosa imani nae. Asubuhi ya leo gazeti maarufu la michezo nchini Mwanaspoti limeripoti kwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Jackson Mayanja kuvunja mkataba wake na timu hiyo na kumwacha bosi wake Omog.
Ukiondoa hayo , bado timu hiyo imeanza kukumbana na adha ya majeruhi kwa wachezaji wake; Kipa Nduda , mshambuliaji John Bocco , mlinzi Shomari Kapombe ambaye toka asajiliwe hajacheza kutokana na majeruhi . Wa nne ni beki wa kutumainiwa Salumu Mbonde.
AMEANDIKA Samel samuel
Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba na krejea kwao Uganda. Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.


kwa upande wake kocha huyo msaidizi amesema haya;

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema. Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF