KUELEKEA KARIAKOO DERBY YANGA NA SIMBA
KUELEKEA KARIAKOO DERBY........
YANGA SC
Huu ni mwendelezo wa makala ya awali juu ya joto la mechi ya watani wa jadi jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Baada ya kuitazama Simba SC kiundani sasa tuwaangazie mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara ambao ndio watakuwa wenyeji wa mechi hiyo dhidi ya mahasimu wao Simba SC.
Kama ilivyo Simba, Yanga pia wanaingia katika mechi hii wakiwa na mtaji mzuri kisaikolojia , kimbinu , kiufundi, ari ya kupambana na hamasa kubwa ya kulinda heshima yao ya soka nchini kama mabingwa mara tatu mfululizo pia wakitaka uongozi wa ligi baada ya kulingana pointi sawa na Simba lakini Simba wakiongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga .
LWANDAMINA
Huyu ndio kocha mkuu wa Yanga ambaye anaingia kwenye mtanange huu akiwa na pressure kubwa kushinda mechi ya derby baada ya kucheza mechi tatu na kuambulia patupu baada ya kufungwa mechi tatu. Lwandamina msimu wa 2016-17 alianza na kupoteza 2-1 na Simba SC. Kwenye michuano ya Mapinduzi alifungwa na Simba kwenye mikwaju ya penati hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Lwandamina na vijana wake katika mechi ya ufunguzi ligi kuu msimu wa 2017-18 al maarufu kama Ngao ya jamii alipoteza pia kwa mikwaju ya penati hali inayomfanya kabla ya mechi ya jumamosi kuwa na rekodi ya kufungwa mechi tatu na Simba SC na kuambulia sare moja!.
Rekodi hiyo inamfanya George Lwandamina kuingia kwenye Kariakoo Derby akiwa na pressure kubwa kuhitaji matokeo chanya ili kuwaaminisha wapenzi na wanachama wa timu hiyo uwezo wake wa kucheza mechi za Derby kama alivyokuwa Zambia na kikosi cha Zesco United. Umakini , uwezo wa kuisoma Simba , kuandaa vyema kikosi chake ni vitu pekee ambavyo vinaweza kumfanya kushinda mchezo huo na kujipa thamani mpya mbele ya wanachama . Raha ya ubingwa kwa timu hizi mbili ni mmoja kumfunga mwenzake .
Kifalsafa Lwandamina ni muumini mzuri wa soka la kushambulia linalochezwa kwa pasi fupi fupi zenye kasi zikihama kutoka box moja kwenda jingine kwa njia ya kati ambayo inawatumia walinzi wa kati , viungo wa kati na mshambuliaji kiongozi nyuma ya playmaker wa juu anaetengeneza daraja kati ya viungo na mshambuliaji wa kati. Aliwapumzisha Kelvin Yondani na Juma Abdul mchezo wa juzi dhidi ya Stand United kutokana nakuwa na kadi mbili za njano. Kama wangepata kadi kwenye mechi ile ni dhahiri mchezo wa jumamosi wangeukosa ! . Lwandamina humtumia Yondani kama mlinzi kiongozi wa kati ambaye ana uwezo wa kukaba na kushirikiana vyema na kiungo wa chini kuanzisha mashambulizi aidha kupiga mipira mirefu kwenye wings ( fast break / outer ) au give and go passes kuwatafutia mwendo viungo wa kati . Yondani anaetengeneza kombinesheni nzuri na sweeper Vincent Andrew pia ana uwezo wa kuwapanga vyema walinzi wa pembeni aidha kwenye mtego wa kuotea au kufanya marking hususani kuziba njia kabla ya mpira kufika.
Lwandamina ambaye msimu uliopita akiwa na Juma Mwmbusi kama kocha wake msaidizi aliyempokea toka Hans van der Pluijm , aliendeleza falsafa ya kushambulia kupitia pembeni kupitia mawinga kama Saimoni Msuva ambaye hivi sasa ametimkia Al jadida ya Morocco pia Deusi Kaseke wing ya kushoto. Lakini msimu huu baada ya mabadiliko makubwa ya kikosi hicho kwa wachezaji wengi kuondoka na wapya wengi kuingia , Lwandamina amebadili mifumo na mbinu zake kulingana na aina ya wachezaji alionao . Ukiitazama Yanga hivi sasa si timu ambayo inategemea tena wings kutafuta magoli. Yanga inaweka soka chini ambalo linasonga mbele kwa kutandaza mpira chini kutoka box moja kwenda jingine. Katika mechi 5 za awali ligi kuu msimu huu timu ilionekana kukosa kasi , uchache wa kutengeneza nafasi za kufunga pia ubutu wa safu ya ushambuliaji kufunga. Mechi mbili za mwisho dhidi ya Kagera Sugar na Stand United, timu imekuwa na nguvu , kasi , uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za kufunga na kufunga huku mfumo ukiruhusu kila mchezaji kucheza kwa uhuru na kujituma. Katika mechi mbili za mwisho Lwandamina akitumia 4-3-3 amepata magoli 6 ! akiwachapa Kagera 2 na kushinda 4-0 dhidi ya Stand United.
Eneo la kiungo amelifungua kunyumbuka katika kujenga mashambulizi pia kuilinda timu katika kushambuliwa. Pappy Tshishimbi licha ya kusimama kama kiungo mkabaji lakini takribani mechi mbili anamtengeneza kama kiraka akiwa uwanjani . Anatibua mipango ya wapinzani kuanzia juu, hushuka chini kukaba lakini pia hutanua kiungo kujilinda kwenye wings ili kuwakataa wapinzani kupitia pembeni ' huru' kushambulia. Mechi na Kagera alimpanga juu kama kiungo mchezeshaji lakini na majukumu mawili kuhakikisha kiungo cha wapinzani wao hakisogei , hakitulii kupanga timu , kumsaidia Makapu kwenye blocking pia kumzunguka Ajibu acheze huru kwenye final third kama ' screening ' kwenye attacking pattern ndio maana kuna wakati Tshishimbi alikuwa anafanya driving kwenye final third ili Chirwa na Ajibu wafunguke kitu ambacho kilikuwa kinawafanya Stand kurudi nyuma sana na kuvuka kwenye marking zone yao. Hili pia siku ya jumamosi inawezeka akicheza na Rafael Daudi au Kamsoko kama atakuwa amepona.
Piusi Buswita ni mtaji mwingine kwa Lwandamina kwenye wings , hachezi kama winga teleza Saimoni Msuva kwa maana ya ' sprinting ' . Buswita kulingana na mfumo wa Lwandamina kwa sasa unaotumia pasi fupi fupi ( box to box ) anachezeshwa kama kiungo mchezeshaji wa pembeni anaeukata uwanja anaposhambulia kwa maana ya kuongeza mashambulizi makali ya kati kuwazunguka Ajibu na Chirwa sasa hili huwalazimisha wapinzani hususani walinzi wa pembeni kusogea kati na kuziacha wazi flanks ambazo Ajibu au Chirwa hutanua pembeni kwa ajili ya counter . Simba wasipokuwa makini na mfumo huu kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kucheka na nyavu.
Driving force ya Ajibu ambaye kwa sasa anachezeshwa kama mshambuliaji mchezeshaji ( playmaker ) ina faida kubwa kwa Yanga kutengeneza set pieces au ku unlock muhimili wa ulinzi kutokana na uwezo mkubwa wa kukokota mpira pia kuuficha mpira. Licha ya uimara wa kiungo cha chini cha Simba SC lakini bado sio wazuri sana kukabia juu au kuvunja mipango ya wapinzani kabla haijafika kwenye attacking zone , endapo wakimruhusu Ajibu na back up ya viungo wa kati na pembeni kuwa huru kwenye eneo lao la ulinzi hakika Yanga inaweza kucheka na nyavu kwa kuutazama mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa waliopata shida kuwazuia kwenye eneo lao la mwisho.
Wing ya kulia ya Simba SC kama atapangwa Erasto Nyoni na Shiza Kichuya , Lwandamina kuna uwezekano mkubwa wing yake ya kushoto kuendelea kumwamini Gadiel Michael na Mwashiuya ambayo kwenye edge juu wanapata sapoti ya Ajibu kwenye attacking patterns huku kwenye marking Tshishimbi kama kiungo kiongozi kati hufika kutibua au kuziba njia . Erasto mzuri kupanda na kushuka hivyo ni lazima wing iwe technical weight kubwa kumlazimisha kubaki chini kitu ambacho Lwandamina anakiweza kwa kufanya swtiching za namba mara kwa mara kati ya Ajibu , Chirwa na Mwashiuya kwenye pressing .
Sina shaka na uwezo wa Youthe Rostand kwenye lango la Yanga . Ana uwezo mzuri kucheza krosi na kucheza one against one. Kikubwa lazima aongee na walinzi wake wa kati kuziba vyema njia ya kati ambayo kinara wa mabao ligi kuu Emanuel Okwi ni fundi wa kuitumia. Wakiweza kumzuia Haruna Niyonzima kuchezesha timu na kuficha mipira pia wakimziba Mzamiru au Ndemla kulingana na seletion ya Omog basi watamfanya Okwi acheze chini zaidi kama deep playmaker kitu ambacho kitawafanya Yondani na Dante kuwa huru kama wataanza katika pacha hiyo.
USIKOSE MAKALA IJAYO
SAMUEL SAMUEL
Comments
Post a Comment