ABDI BANDA AZIDI KUAMINIWA BAROKA FC SAUZ
Timu ya Abdi Banda ligi kuu nchini Afrika Kusini, Baroka FC walazamishwa sare na Golden Arrows . Banda ameendelea kutumika kikosi cha kwanza toka atue timu hiyo mapema mwanzoni mwa msimu huu.
Baroka walipata goli mapema dakika ya 15 kupitia kwa Moeti lakini Golden Arrows walichomoa dakika ya 75 kupitia Magubane.
Vikosi vyote vilikuwa hivi;
Baroka FC: Vries, Mothupa, Shaku, Mdatsane, Masenamela, Banda, Madubanya, Moeti (Kgaswane 68’), Matloga (Sidumo 82’), Motupa, Macha (Nguzana 60’)
Golden Arrows: Gumede, Dube, Mzava, Mngwengwe, Nkombelo, Bilankulu (Shongwe 58’), Cele, Magubane, Mahachi (Mutizwa 71’) , Jooste (Jappie 58’), Lamola
@ SAMUEL SAMUEL
Hata ivyo wadau na wapenzi wa soka nchini wanaombwa kuwaunga mkono vijana wenye vipaji vya kucheza soka kwa hali na mali ili kuwasaidia wapate nafasi ya kucheza soka la kulipwa ili kuisaidia timu ya taifa ya tanzania kimataifa. Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji vya kulisakata soka ila moja ya changamoto ni uchache wa mawakala wenye weledi wa soka.

Comments
Post a Comment