AJIBU AMBWAGA NIYONZIMA KITAKWIMU LIGI KUU

Anaandika shafii D
Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib ni wachezaji waliozungumzwa sana wakati wa dirisha la usajili kabla ya kuanza kwa msimu huu kwa sababu ya kuhama kutoka klabu zao na kujiunga na mahasimu wa klabu walizozihama.
Inatajwa kwamba Ajib alisajiliwa na Yanga kwa Tsh. 50 Mil pamoja na gari ndogo ya kutembelea (Toyota Brevis). Wakati huo ikielezwa Niyonzima ndiye mchezaji ghali kusajiliwa msimu huu baada ya kuvuta mtonyo unaokadiriwa kufika Tsh. 120 Mil.
Baada ya ligi kuanza Ajib ameshafunga magoli matatu na ku-assist moja katika mechi sita alizocheza wakati Niyonzima bado hajafunga wala kutoa assist katika magoli 14 ambayo Simba imefunga hadi dasa.
Hata hivyo Ibrahim Ajibu Alimaarufu ''migomba'' ameaonekana kuzikponga nyoyo za wapenzi wengi wa wa Yanga na kuanza kuwazodoa wenzao wa Simba kwamba wao ndio walio okota bingi kumsajiri Ajibu. lakini pia Haruna aliwakosha wapenzi na wanachama wa simba baada kuisaidia simba kusawazisha katika mechi dhidi ya mtibwa.mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF