BADO MNA MASHAKA NA GL?

BADO MNA MASHAKA NAE?
Anaandika SAMUEL SAMUEL
Moja ya sifa kubwa aliyonayo ni uwezo wa kumtumia kila mchezaji ndani ya kikosi chake kusaka matokeo chanya. Hili linasadifiwa vyema na uwezo kitaaluma katika kufundisha mchezo huu wa soka pia saikolojia yake jadidi katika kumjenga mchezaji kucheza kwa moyo wote.
Mchezo wa leo Lwandamina ameonesha uwezo wa kumsoma mpinzani wake na kutumia nguvu aliyonayo kupambana nae.
Kilipotoka kikosi baadhi ya mashabiki wa Yanga waliingiwa hofu na wengine kumtupia lawama mwalimu. Ni haki yao kuwa na hofu kutokana na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Kagera sugar pia historia mbaya ya kupoteza michezo mitatu ya nyuma huku wakitoka sare michezo miwili hivyo waliamini leo Kagera wangeikamia Yanga.
Lwandamina kaingia Kagera akiwa hana Thaban Kamusoko kwenye kikosi chake . Injini yake ambayo hukiendesha kiungo chake , ni mzuri kwenye eneo la kiungo cha chini pia juu . Mechi na Mtibwa uwanja wa Uhuru licha yakuwa majeruhi ilimlazimu kumtumia kupunguza kasi ya wakata miwa hali ambayo kwa kiasi fulani ilimtonesha zaidi. Aliamua kumuacha Dar es salaam apate matibabu ya kutosha . Alikwisha piga hesabu zake na alijali afya ya mchezaji wake.
Ukimuondoa Kamusoko, Lwandamina pia ameingia Kagera bila Donald Ngoma pia majeruhi yakiendelea kumsonga Amisi Tambwe. Hawa ni wachezaji ambao msimu uliopita na mechi zilizopita walikuwa wakitumika kikosi cha kwanza . Nadhani unapata picha kichwa cha mzambia huyo ambaye mpaka sasa viatu vya Msuva amekosa wa kumkabidhi.
Baada ya kulitambua hilo, Lwandamina aliingia uwanjani akibadilika kabisa na leo amedhihirisha soka ni taaluma sio mali kauli.
Eneo la ulinzi halikuwa na mabadiliko lakini hesabu zake alizipigia kwenye eneo la kiungo na ushambuliaji. Wengi walihisi kukosekana kwa Kamusoko basi ni dhahiri angewatumia Tshishimbi na Rafael eneo la kati lakini aliamua kumtumia Juma Makapu kama kiungo mkabaji wa chini ( deep lying holding midfielder) akiwa na jukumu la kuwalinda walinzi wa kati , kuvunja mipango ya viungo wa kati wa Kagera lakini muda wote akihakikisha njia ya kati kuja kwa Rostand inalindwa vyema.
Jeuri ya kumtumia Makapu ambaye hana tofauti aliipata kutokana na uwezo wa Pappy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu. Alijua fika hata kama Makapu asipotembea mbele lakini yupo Tshishimbi ambaye anauwezo wa kushuka chini kuchukua mipira kuipeleka mbele au kukitanua kiungo ili Ajibu apate nafasi zaidi ya kuingia na kutoka kama deep playmaker kumchezesha Chirwa au yeye mwenyewe kusogea mbele .
Ilikuwa ngumu sana kwenye mfumo wa 4-3-3 awapange Tshishimbi na Daudi kati kwa viungo wenye nguvu kasi na uwezo wa kushambulia wa Kagera Sugar. Daudi hana kasi na si mkabaji, ni mzuri akiwa na mpira lakini si mzuri sana kwenye mfumo au mbinu za mwalimu anaetaka kujilinda na kushambulia.
Makapu alisimama chini na leo aliifanya vyema kazi yake ingawa wengi wanaweza wakawa hawajamuelewa kutokana na kukitaka kiungo kiungo kinachopanda na kushuka . Hii ilikuwa ngumu kutokana na njia ya kati pekee ndio ulikuwa uhai wa Yanga leo kwenye kushambulia pia kulinda .
Endapo wings zingekuwa vizuri, vizuri kwenye kasi ya kushambulia, kuchezesha timu kwa uhakika wa krosi zao kusaidia marking basi ni dhahiri Makapu angeanzia nje na eneo la kiungo wangesimama Tshishimbi na Rafael Daudi . Kiasi Buswita anaendelea kuimarika lakini bado hajafikia kiwango alichokuwa nacho Msuva pia Mwashiuya bado anakosa uhakika wa krosi zake na si wazuri sana kwenye kukaba hivyo Lwandamina alihitaji kuwakamata Kagera kati na kwenye wings kuwaacha walinzi na mawinga hao kupunguza pressure.
Muunganiko wa Makapu, Tshishimbi, Ajibu na Obbrey Chirwa ndio ulikuwa mwiba kwa Kagera.
Kwenye safu ya ulinzi Andrew Vicent na Yondani wameendelea kuimarika makosa madogo tu ya kujisahau kwenye mipira ya juu mfano goli la Kagera kumwacha mfungaji kuruka huru yanatakiwa kurekebishwa.
SAMUEL SAMUEL

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF