HUU NDIO UKWELI KUHUSU LWANDAMINA KUFUKUZWA YANGA

Uongozi wa Yanga kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Clement Sanga umesema kocha wa yanga George Lwandamina yupo salama na hajafukuzwa kama wengi walivyodai katika mitandao ya kijamii. Pia amesisitiza kuwa endapo kutakua lolote taarifa itatolewa.

''Tumeziona taarifa hizo wengi pia wameongea lakini sisi Yanga hatujawahi hata kukaa wala kuhoji uwezo wa kocha mkuu wa Yanga wala kufikiria kufanya mabadiliko ya kocha wetu wa Yanga''alisema Sanga ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya mwenyekiti katika bodi ya ligi.

''Mimi ndiye kiongozi mkuu wa Yanga hivi sasa nasisitiza kwamba hatujawahi kufikiria wala hatuna mpango huo, labda kama kuna watu pembeni wenye fikra hizo lakini sisi kama Yanga hatuna mpango huo kwakua tuna imani kubwa na kocha wetu Lwandamina''. Sanga ambae pia ndiye mwenyekiti wa kilabu hiyo tangu kuondoka kwa Yusuph Manji.

Kunaweza kukawa na mapungufu madogo ambayo uongozi tumeuona na tunaufanyia kazi, lakini kuhusu mabadiliko ya  hatujakaa kikao chochote kujadili swala hilo. labda kama kuna yanga nyingine huko pembeni ila sisi yanga tunaimani kubwa Lwandamina

Comments

Popular posts from this blog

Education for liberation and self-reliance By J.K.NYERERE

MABINGWA LIGI KUU TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWA LIGI KUU 1965

MALALAMIKO MCC KUHUSU GOLI LA KICHUYA YATU BODI YA LIGI NA TFF