ULINGANISHO SAHIHI WA MAFUNDI WA SOKA WA YANGA NA SIMBA
Mkitaka mjadala wenu wa ulinganifu uwe na mashiko zaidi , uwekeni hivi;
1. Ibrahim Ajibu vs Emanuel Okwi
2. Niyonzima vs Kamusoko
Niyonzima kwa Ibrahim Ajibu hapana hususani kwenye ufungaji. Unaweza kuwaweka kwenye mizani sawa ya upigaji wa pasi za mwisho pia kubadili mfumo wa ushambuliaji lakini Ajibu na Okwi wana kitu cha ziada kwa Niyonzima. Hawa ni wafungaji wazuri , wachezeshaji na wana uwezo mkubwa kuibeba timu wao kama wao hususani kwenye mazingira tata ya kuamua matokeo.
Niyonzima bado yupo katika kundi la kati la viungo ambao primary role ni kuchezesha zaidi timu . Anaweza asipige pasi ya mwisho lakini akasidia ' holding ' kwenye low midfield zone na playmakers hawa kina Ajibu na Okwi wakapata nafasi ya kuja kati kuuchukua mpira kwenda mbele kumchezesha mshambuliaji wa kati au kupiga tokea mbali au kuwachezesha viungo wa pembeni ambao wana uwezo wa kuikata final third kutokea pembeni.
Si kila kiungo wa juu anaepangwa namba 10 ni mfungaji. Mwalimu anaweza kumpanga juu acheze kama ' kiungo ' huru huku kiungo wa chini yake ( namba 8 ) akasimama kama kiungo mshambuliaji kificho na akawa anashambulia tokea hapo hususani kama anaweza kupiga mashuti ya mbali, kimbinu hupangwa kwa ajili ya counter plans au kucheza second balls kwenye 18 yard ya timu pinzani. Mfano mzuri ni Saidi Ndemla na Mzamiru Yassin wa Simba SC au Kamusoko kipindi cha Hans van der Pluijm .
Comments
Post a Comment