Michuano ya CECAFA kuanza kutimua vumbi Novemba 25
Michuano ya CECAFA kuanza kutimua vumbi Novemba 25.
Mashindano ya kombe la Afrika Mahariki na Kati (CECAFA) yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 9 mwaka huu, huku timu za Zimbabwe na Libya zimealikwa kama wageni kushiriki.
Mashindano haya hayakuandaliwa mwaka jana baada ya wenyeji Sudan kujiondoa na kisha Kenya iliyochukua nafasi ya kuandaa nayo kujiondoa dakika za mwisho.
Nchi zitakazoshiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Sudan kusini, Djibouti, Eritrea, Somalia na Zanzibar.
na samuel samuel
Comments
Post a Comment